Bunge la seneti nchini Haiti limemchagua kiongozi wake Joseph Lambert kuwa mrithi wa muda wa rais aliyeuawa hivi karibuni, Jovenel Moise.Lakini bunge hilo la seneti halijakuwa na idadi ya kutosha tangu Januari 2020 hivyo basi haiko wazi iwapo Lambert anaweza kuchukuwa madaraka hayo.
Kutokana na kufutwa kwa uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanywa mwezi Oktoba mwaka 2019, ni maseneta 10 tu kati ya 30 walioko ambao muda wao wa kuhudumu haujafikia kikomo.
Pia kumekuwa na hali ya mchanganyiko kuhusu wadhifa wa waziri mkuu wa mpito kufuatia mauaji ya Moise.
Siku ya Jumatatu, Moise alimchagua daktari wake Ariel Henry katika wadhifa huo na akatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatano lakini hafla hiyo ikafutiliwa mbali baada ya mauaji ya rais huyo.
Hivyo basi Claude Joseph aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na waziri mkuu wa mpito ambaye nafasi yake ilikuwa ichukuliwe na Henry, amejitangaza kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo._

No comments:
Post a Comment