Afisa wa zamani katika wizara ya sheria ya Haiti Joseph Felix Badio anashukiwa kuwa ndiye aliyetoa amri ya kuuwawa kwa rais wa taifa hilo Jovenel Moise.
Hayo yameelezwa na mkuu wa polisi wa Colombia Jorge Vargas jana, katika matokeo ya uchunguzi wa awali juu ya mauaji hayo. Moise aliuwawa kwa kupigwa risasi wakati washambuliaji walipovamia makaazi yake binafsi mnamo Julai 7.
Uchunguzi unaofanywa na mamlaka za Haiti na Colombia kwa kushirikiana na jeshi la kimataifa la Interpol juu ya mauaji hayo, umebaini kuwa Badio anaonekana alitoa agizo la mauaji siku tatu kabla ya shambulio hilo.
Taarifa zaidi zinasema afisa huyo aliwaamuru wanajeshi wa zamani wa Colombia Duberney Capador na German Rivera kumuua rais Moise. Capador aliuwawa na Rivera alikamatwa na polisi wa Haiti.

No comments:
Post a Comment