Msanii Mkongwe wa Muziki wa Rap Duniani kutokea Nchini Marekani Biz Markie amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57
Kwa Mujibu wa @tmz_tv Nguli huyo Biz amefariki Ijumaa katika hospitali ya Baltimore alipokuwa akipatiwa Matibabu, #BizMarkie alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sukari kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Miongoni mwa kazi za Nguli huyu #BizMarkie ni pamoja na "Just a Friend", "Make the Music with Your Mouth Biz," "Nobody Beats the Biz," "Vapors," na nyingine kibao.
No comments:
Post a Comment