Search This Blog

Friday, June 25, 2021

Yanga mzigoni dhidi ya Biashara United leo


Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kikitarajiwa kushuka Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United leo.

Mchezo wa leo ni wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho  na mshindi wa leo atacheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC na Simba utakaochezwa kesho, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Nyota hawa wa yana wataukosa mchezo huo ni pamoja na Lamine Moro, Michael Sarpong, Metacha Mnata hawa kutokana na masuala ya nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha na Abdalah Shaibu, 'Ninja' hawa bado hawajawa fiti kutokana na kutibu majeraha yao.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasihaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa Balama, Ninja maendeleo yao ni mazuri.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...