Search This Blog

Friday, June 25, 2021

UEFA yatangaza kufuta bao la ugenini

 


SHIRIKISHO la Soka Ulaya (Uefa) limetangaza kufuta sheria ya bao la ugenini ambayo ilikuwa inatumika kwenye michuano ambayo inaandaliwa na Uefa sheria hiyo ilianza kutumika tangu mwaka 1965.

Sheria hiyo ilikuwa inatumika kuamua matokeo baada ya raundi mbili  nyumbani na ugenini, baada ya kufuta sheria hiyo na baada ya kuchezwa  raundi mbili, endapo   matokeo yakiwa sare, basi zitaongezwa dakika 30 na baadaye mikwaju ya penati.

Timu kadhaa ikiwemo Chelsea, Manchester City na PSG kwa nyakati tofauti walikuwa wahaga wa sheria hiyo  baada ya kujikuta wakitupwa nje ya michuano kutokana na timu pinzani kunufaika  kwa faida ya goli la ugenini.

Kwa mujibu wa Rais wa Uefa Aleksander Ceferin amesema goli la ugenini limefanya timu nyingi kucheza kwa kujilinda kwa sababu ya faida ya bao la ugenini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...