“Mfumuko wa bei umeendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja ambapo ulipungua kutoka wastani wa 3.4% mwaka 2019 hadi 3.3% mwaka 2020, mfumuko wa bei umebaki katika wigo wa 3.3% Mei 2021” - Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba akisoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendelo wa Taifa wa mwaka 2021/22.
“Mwenendo wa mfumuko wa bei umeendelea kuwa tulivu kutokana na upatikanaji wa chakula cha kutosha, kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani na sarafu nyingine duniani na usimamizi madhubuti wa sera za fedha na bajeti” - Nchemba.

No comments:
Post a Comment