“Licha ya mlipuko wa Covid-19 ulioathiri uchumi wa Nchi nyingi duniani, Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache duniani zilizokuwa na ukuaji chanya wa uchumi kwa mwaka 2020, Pato la Taifa lilikua kwa 4.8% ikilinganishwa na ukuaji wa 7.0% mwaka 2019, ukuaji chanya ulitokana na hatua ya Serikali ya kuruhusu shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea na wakati huohuo Wananchi wakisisitizwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya” - Waziri Nchemba
“Aidha, kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini kulichangiwa na athari za Covid-19 katika nchi washirika wa kibiashara pamoja na mafuriko yaliyosababisha uharibifu wa miundombinu ya usafirishaji na kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo”— Waziri Nchemba
“Athari za Covid- 19 zilijitokeza zaidi katika shughuli za kiuchumi za malazi, huduma ya chakula pamoja na sanaa na burudani ambazo zilikuwa na ukuaji hasi kwa mwaka 2020” — Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba akisoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendelo wa Taifa wa mwaka 2021/22.

No comments:
Post a Comment