Search This Blog

Sunday, June 20, 2021

Waziri Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wapya Jumatatu

 


Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa wote nchini kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu June 21, 2021 huku akisema kusiwe na kisingizio chochote.

Akizungumza leo Dar es Salaam Waziri Ummy amesema-“Kama kuna sababu yoyote basi Jumanne zoezi liwe limekamilika kwasababu tunataka hadi Jumatano Wakuu wa Wilaya wote wawepo katika vituo vyao vya kazi, waende wakaripoti katika vituo vyao vya Kazi halafu baadaye ndio wanaweza kurudi kwa ajili ya taratibu za kuhama”



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...