Search This Blog

Sunday, June 20, 2021

Idadi ya vifo Brazil yapita 500,000 kufuatia COVID-19

 


Brazil imekuwa taifa la pili duniani baada ya Marekani ambayo idadi yake ya vifo kutokana na janga la COVID-19, imepitiliza 500,000.

Ongezeko hilo la idadi ya vifo katika taifa hilo la kusini mwa Amerika, linajiri mnamo wakati nchi hiyo inakumbwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona.

Wizara ya Afya iliripoti jumla ya vifo 500,800 ikiwa ni pamoja na watu 2,301 waliofariki ndani ya saa 24 zilizopita.

Hayo yakijiri, maelfu ya waandamanaji walijitokeza katika mji wa Rio de Janeiro na miji mingine kadhaa kulalamika kuhusu namna rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro anavyolishughulikia janga la virusi vya corona.

Wamemshtumu kwa kutonunua chanjo za virusi hivyo kwa haraka na pia ukaidi wake dhidi ya kuvaa barakoa.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...