Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo lililofadhaika na chaguzi nne katika kipindi cha miaka miwili ya kukwama kisiasa.
Alisema serikali yake "itafanya kazi kwa ajili ya watu wote", akiongeza kuwa vipaumbele vitakuwa mageuzi katika elimu, afya na kupunguza taratibu nyingi za serikali.
Mzalendo huyo wa mrengo wa kulia ataongoza muungano ambao haujawahi kutokea wa vyama vinavyoungwa mkono na wabunge katika kura ya Jumapili iliyoishia 60-59.
Anamrithi Benjamin Netanyahu ambaye alilazimishwa kuondoka ofisini baada ya miaka 12.
Bwana Bennett, kiongozi wa chama cha Yamina, atakuwa waziri mkuu hadi Septemba 2023 kama sehemu ya makubaliano ya kugawana madaraka.
Halafu atamkabidhi Yair Lapid, mkuu wa karist Yesh Atid, kwa miaka miwili zaidi.
Bwana Netanyahu - waziri mkuu wa Israeli aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi - atabaki kuwa mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud na kuwa kiongozi wa upinzani.
Wakati wa mjadala wa Jumapili huko Knesset (bunge) huko Jerusalem, Bw Netanyahu aliahidi: "Tutarudi."
Baada ya wabunge kupiga kura katika serikali mpya ya muungano, Bw Netanyahu alimwendea Bwana Bennett na kumpa mkono.
Katika hotuba yake, Bwana Bennett, 49, alisema: "Hii sio siku ya maombolezo. Kuna mabadiliko ya serikali katika demokrasia. Ndio tu.
"Tutafanya kila tuwezalo na hakuna mtu anayepaswa kuhofu ... . "
Wawakilishi wa Wapalestina wametoa maoni kuhusu serikali mpya ya Israeli.
"Hili ni jambo la ndani la Israeli. Msimamo wetu umekuwa wazi kila wakati, tunachotaka ni serikali ya Palestina kwenye mipaka ya 1967 na Jerusalem kama mji mkuu wake," msemaji wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema.
"Ni kazi na taasisi ya kikoloni, ambayo tunapaswa kuipinga kwa nguvu ili kurudisha haki zetu," alisema msemaji wa Hamas, kundi la Kiislam linalodhibiti Gaza.
Rais wa Marekani Joe Biden alituma pongezi zake kwa Bwana Bennett, akisema anatarajia kuimarisha uhusiano wa "karibu na wa kudumu".

No comments:
Post a Comment