Watu 2 waliuawa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa katika eneo la soko huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.
Afisa wa Polisi wa Mogadishu Abdifatah Hassan alitangaza kuwa shambulizi la bomu lilitekelezwa katika soko dogo huko Ex-control Afgoye, lililoko mji mkuu wa Mogadishu.
Akibainisha kuwa watu 2 walipoteza maisha katika shambulizi hilo, Hassan alisema,
"Tunashuku mhusika wa shambulizi hilo alikuwa mshambuliaji aliyevaa vazi la kujitoa muhanga."
Hassan alifahamisha kuwa vikosi vya usalama vilitumwa katika eneo la tukio na uchunguzi ulianzishwa.
Kwa upande mwingine, katika taarifa za vyombo vya habari vya kitaifa, ilitangazwa kuwa watu 8 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo na walikuwa wakitibiwa.
Hakuna mtu yeyote ambaye amedai kuhusika na shambulizi hilo.
Shirika la kigaidi la Al-Shabab mara kwa mara huandaa mashambulizi yakilenga vikosi vya usalama na makaazi ya raia nchini Somalia.

No comments:
Post a Comment