Search This Blog

Thursday, June 24, 2021

Ujerumani yashauri Ulaya kuzungumza na Urusi


Ujerumani imependekeza kwa Umoja wa Ulaya kufanya mkutano wa kilele na Rais Vladmir Putin wa Urusi kama sehemu ya mkakati mpya wa kushughulikia uhusiano kati ya pande hizo mbili. 

Akilihutubia bunge la Ujerumani, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kutafuta mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Putin hata wakati ukisimama pamoja dhidi ya uchokozi kutoka Urusi, na kuongeza kuwa haitoshi tu kwa rais wa Marekani kuzungumza na rais wa Urusi. 

Wakiwa pande kinzani katika mikwamo nchini Ukraine na Belarus, na mikwaruzano kuhusu haki za binadamu, Umoja wa Ulaya na Urusi zinashutumiana kwa kuingilia kati uchaguzi, kampeni za upotoshaji na kutishia usalama na utulivu kuanzia mataifa ya Baltic hadi Bahari Nyeusi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...