Vyombo vya habari vya Ivory Coast vinaripoti kwamba rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo amempa talaka mke wake na mshirika wake wa Simone Gbagbo, siku kadhaa baada ya kurejea katika taifa hilo la Afrika magharibi akitokea Ubelgiji.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa kibinafsi , wakili wa Laurent Gbagbo Claude Mentenon alisema kuwa Gbagbo alikuwa anataka kumtaliki Simone baada ya"kukataa mara kwa mara kwa miaka mingi" kwa mama huyo "kukubali kuachana naye ".
Wote wawili walishitakiwa ba Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa uhalifu unaohusiana na mzozo uliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na 2011, lakini walipatikana bila hatia.
Wakatimumewe alipokuwa hayupo nchini, mara kwa mara Simoni aliunga mkono na kutoa wito wa kurejea kwake nchini.
Laurent Gbagbo, mweye umri wa miaka 76, amekuwa akiishi Nady Bamba, mwandishi wa zamani wa habari mwenye umri wa miaka47-kwa miaka mingi. Alirejea naye nchini Ivory Coast tarehe 17 Juni.

No comments:
Post a Comment