Search This Blog

Tuesday, June 22, 2021

Rais wa Ufilipino atishia kuwafunga wanaokataa chanjo


Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino ametishia kuwafunga jela watu watakaokataa kupata Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19 wakati Taifa hilo likipambana na mlipuko mbaya zaidi Barani Asia.

Kufuatia Ripoti za idadi ndogo ya wanaojitokeza katika Vituo mbalimbali vya Chanjo Jijini Manila, Rais amesema watu waamue kupata Chanjo au atalazimika kuwapeleka gerezani.

Kauli yake inakinzana na ile ya Maafisa wake wa Afya ambao wamesema licha ya kwamba Wananchi wanasisitizwa kupata Chanjo, suala hilo ni hiari.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...