Search This Blog

Tuesday, June 15, 2021

Rais Samia kuzungumza na vijana leo


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Juni 15, 2021 anatarajia kukutana na kuzungumza na vijana wa Kanda ya Ziwa kwa niaba ya vijana wa Tanzania katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Tangu amekuwa kiongozi mkuu wa nchi, Samia amekutana na makundi mbalimbali na kupokea maoni yao, changamoto na namna ya kuzitatua na katika mkutano huo anatarajia kukutana na vijana zaidi ya 1,000.

Mamia ya vijana kutoka Mikoa ya Kanda hiyo tayari wamewasili uwanjani hapo kuanzia saa 12 asubuhi huku kukiwa na misururu ya vijana wengine nje ya uwanja wakisubiri kukaguliwa kwa ajili ya kuingia ndani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...