Search This Blog

Saturday, June 12, 2021

Raia wa Algeria wapiga kura ya bunge


Waalgeria wanaendelea kupiga kura katika uchaguzi wa bunge ulioanza hii leo baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema asubuhi. 

Ni uchaguzi ambao utawala nchini humo unatumai utafungua ukurasa mpya wa matumaini kufuatia miaka miwili ya mgogoro wa kisiasa, lakini pia raia wengi wanatarajiwa kuususia. 

Rais Abdelmadjid Tebboune ametoa wito kwa raia kushiriki katika uchaguzi huo wa bunge lakini bado Wa-algeria hawana hamu ya kupiga kura kutokana na kile wanachoamini kwamba nchi hiyo inaoongozwa na jeshi pamoja na vikosi vya usalama. 

Kwenye kituo kimoja cha kupigia kura katika shule moja ya msingi karibu na ofisi ya Waziri Mkuu Abdelaziz Djerad, polisi kadhaa walionekana kushika doria na dakika chache kabla ya kituo hicho kufunguliwa ni watu watano tu waliokuwa nje wakisubiri kupiga kura.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...