Polisi ya Nicaragua imemweka chini ya kizuizi cha nyumbani mwanasiasa kinara wa upinzani Cristiana Chamorro baada ya serikali kudai anahusika na utakatishaji wa fedha.
Taarifa iliyotolewa na famiia ya mwanasiasa huyo imesema polisi walivamia nyumba ya Chamorro iliyopo kwenye mji mkuu wa Nicaragua na kufanya upekuzi kwa saa tano kabla ya kumweka chini ya kizuizi cha nyumbani.
Chamorro mwenye umri wa miaka 67 anazingatiwa kuwa mpinzani mkuu wa rais Daniel Ortega katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Novemba.
Mapema jana mahakama moja ya mji mkuu Managua ilisema imeamuru kukamatwa kwa mwanasiasa huyo kwa makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na mali na kuidhoofisha serikali ya Nicaragua.

No comments:
Post a Comment