Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amewatoa hofu Watanzania kuhusu picha zinazoonekana mitandaoni zikionesha makontena ya makinikia yameanza kusafirishwa kupeleka nje ya nchi, na kusema kuwa hayo yanayoonekana yameshauzwa na serikali imekwishachukua fedha zake.
Kauli hiyo ameitoa Bungeni leo Juni 3, 2021, wakati akijibu swali la Mbunge wa Msalala, Mhe. Iddi Kassim Iddi, aliyehoji kuhusu makontena ya makinikio ambayo yamekuwa yakionekana katika njia ya Bulynhulu Kahama na bandari ya Dar es Salaam yakisafirishwa kupelekwa nje ya nchi ili hali serikali mwaka 2018 ilizuia usafirishaji wa makinikia hayo.
"Na mimi pia nimeona kwenye mitandao kwamba watu wanaona makontena ya makinikia yakisafirishwa kwenda nje, niwatoe hofu Watanzania hayo wanayoyaona yameshauzwa na mnunuzi anakuwa huru kuyapeleka anapotaka, kwahiyo waondoe mashaka hakuna kontena linalotoka nchini bila kuuzwa," ameeleza Waziri Mkuu Majaliwa wakati akijibu swali hilo.

No comments:
Post a Comment