Shirika la Madaktari wasio na mipaka (MSF) wamesema kuwa wameshtushwa na mauaji ya kikatili ya wafanyakazi wake watatu kaskazini mwa Ethiopia, mji wa Tigray.
Kundi hilo la misaada ya dawa limesema walipoteza mawasiliano na kikosi chao wakati wakisafiri Alhamisi mchana.
Miili ya wafanyakazi wawili raia wa Ethiopia na mmoja raia wa Uhispania ilipatikana Ijumaa asubuhi mita chache kutoka katika gari lisilokuwa na kitu.
Kundi hilo lilijumuisha :
Maria Hernandez, mwenye umri wa miaka 34, raia wa Spain - alikuwa mratibu wa masuala ya dharura aliyeanza kufanya kazi MSF mwaka 2015
Yohannes Halefom Reda, mwenye umri wa miaka 31, kutoka Ethiopia - mratibu msaidizi aliyejiunga na MSF mwezi Februari.
Tedros Gebremariam Gebremichael, miaka 31 pia kutoka Ethiopia - alikuwa dereva aliyejiunga MSF mwezi Mei.
"Hakuna maneno yanaweza kueleza masikitiko yao yote, mshtuko walioupata kutokana na shambulio hili baya ," MSF ilisema kwenye taarifa yake.
"Maria, Yohaness na Tedros walikuwa Tigray wakitoa msaada kwa watu na inahuzunisha sana malipo yake ni kuuawa,"aliongeza.
Hakuna taarifa juu ya wahusika waliotekeleza shambulio hilo.
Taarifa kutoka serikali ya Ethiopia inawalaumu wale ambao inawaita kundi lisilojua kuwajibika - ikimaanisha waasi ambao wamekuwa wakipigana tangu mwezi Novemba.
Ilipendekeza kuwa shambulio hilo limethibitisha kuwa serikali ilikuwa sahihi kutoa wito kwa mashirika ya kibinadamu kuandamana na wajeshi.
Miezi yote nane ya ghasia katika eneo lote la Tigray limeshutumiwa ukatili dhidi ya raia.
Wiki hii mapigano mjini Tigray yaliongezeka.
Vikosi vya waasi vimesema kuwa vimevamia baadhi ya maeneo ya mjini, na jeshi la Ethiopia lilifanya mashambulizi ya anga , na kuripotiwa kuuwa watu kadhaa.

No comments:
Post a Comment