Search This Blog

Wednesday, June 9, 2021

Makumi ya watoto 'wametekwa na wanamgambo wa kijihadi' Msumbiji


Zaidi ya watu 700,000 , nusu yao watito wamefurushwa makwao kutokana na ghasiaImage caption: Zaidi ya watu 700,000 , nusu yao watito wamefurushwa makwao kutokana na ghasia

Makumi ya watoto, wengi wao wasichana, wametekwa na makundi yakijihadi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Shirika la Uingereza la kuwahudumia watoto, Save the Children linasema.

Shirika hilo limeongeza kuwa karibu watoto 51 wametekwa licha ya ghasia ba ukosefu wa usalama kuwasambaratisha maelfu ya watu.

Linasema idadi ya waliotekwa huenda ikawa "juu zaidi" - kwani ripoti yake inaangazia visa vilivyoripotiwa pekee.

Shirika hilo limeelezea wasi wasi wake kuwa visa vya utekeji "ni mbinu mpya inayotumiwa na mara kwa mara na makundi hayo vitani ".

"Kutekwa, kushuhudia utekaji na kulazimishwa kutoroka mashambulio kutoka kwa makundi ya wanamgambo - ni hali inayowaathiri watoto wadogo kwa wakubwa," mkurugenzi wa shirika hilo nchini Msumbiji Chance Briggs alisema.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...