Uamuzi huo wa mahakama una maana kuwa Mladic amepoteza rufaa yake ya mwisho dhidi ya hukumu yake kwa mauaji ya kimbari. Mladic, mwenye umri wa miaka 78, ambaye baadae alifahamika kama "Mchinjaji wa Bosnia" wakati wa Vita vya Bosnia vya mwaka wa 1992 hadi 95, alitaka afutiwe mashitaka.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewashukuru majaji na wale waliohusika katika kesi hiyo kutokana na bidii yao kwa miongo mingi. Muendesha mkuu wa mashitaka wa mahakama hiyo Serge Brammertz aliukaribisha uamuzi huo na kuwaambia wafuasi wa Mladic kuwa ni wakati wa kukubali ukweli.

No comments:
Post a Comment