Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemuidhinisha Antonio Guterres kuhudumu kwa muhula wa pili, huku utatuzi wa migogoro ukitarajiwa kuwa kipaumbele chake katika uongozi wa shirika hilo la kimataifa.
Guterres mwenye umri wa miaka 72 ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Ureno amekuwa usukani tangu 2017 na hakukabiliwa na ushindani katika kuwania muhula mwingine.
Karibu watu wengine 10 pia walitaka wadhifa huo, lakini hawakuwa wagombea rasmi kwa sababu hakuna yeyote kati ya mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa aliyewaidhinisha. Idhini kutoka kwa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa ni kama suala la utaratibu tu na inatarajiwa kutolewa karibuni.
Wakati wa muhula wake wa kwanza Guterres alilazimika kuangazia zaidi juhudi za kupunguza uharibifu wa maamuzi ya upande mmoja, siasa kali za kizalendo na sera za kigeni zenye wasiwasi za aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump.

No comments:
Post a Comment