Search This Blog

Sunday, June 13, 2021

Kigoma, Mtwara na Ruvuma watia fora riadha maalum


Na Mathew Kwembe, Mtwara.

Wanariadha mahiri kutoka mikoa ya Kigoma, Mtwara na Ruvuma wametia fora katika fainali za mbio za mita 100 za riadha maalum ambazo zimefanyika leo asubuhi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara.

Wanariadha kutoka mikoa hiyo walijizolea medali nyingi kuliko mikoa mingine iliyoshiriki fainali hizo maalum za UMITASHUMTA kwa mwaka huu 2021 ambapo kila mkoa wanariadha wake sita walijishindia medali baada ya kushika mojawapo kati ya nafasi nne za juu kwenye mashindano hayo.

Mikoa iliyofuatia kwa kupata medali nyingi ni Mwanza, Lindi, Mbeya, Njombe, Tabora, Morogoro, Tanga, Pwani na Kilimanjaro baada ya wanariadha watano kutoka kila mkoa huo kujizolea medali maalum.

Wanariadha wanne kutoka mkoa wa Arusha nao walijizolea medali maalum baada ya kushika nafasi nne za juu za fainali hizo.

Mkoa wa Arusha ulifuatiwa na wanariadha kutoka mikoa ya Singida, Iringa na Manyara ambao kila mmoja ulijizolea medali tatu.

Mikoa ya Songwe, Rukwa na Shinyanga kila mmoja ulitoa wanariadha wawili waliopata medali huku mikoa ya Dar es salaam, Dodoma na Geita ikifanikiwa kupata medali moja kwa kila mkoa.

Mbali na mbio za mita 100 fainali maalum  pia kulikuwa na mbio za mita 100, wavulana na wasichana hatua makundi,  kurusha tufe kwa wavulana na wasichana, mbio za mita 200, mita 1500 na mbio za kupokezana kijiti 4 x mita 100 kwa wavulana na wasichana.

Mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga na Mara ilitia fora katika hatua hii kufuatia wanariadha wake wengi kufanya vizuri katika hatua ya mchujo na hivyo kufanikiwa kusonga mbele.

Mashindano ya riadha yaliyoanza leo yataendelea kufanyika hadi tarehe 18/6/2021 ambapo washindi mbalimbali watajinyakulia medali na vikombe.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...