Search This Blog

Thursday, June 24, 2021

Idadi kubwa ya watu wapoteza maisha katika Shambulizi la angani kwenye soko Ethiopia


Idadi kubwa ya watu walipoteza maisha kwenye shambulizi la angani lililotokea katika soko la mkoa wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Ilibainishwa kuwa baada ya shambulizi hilo lililolenga eneo la Togoga mkoa wa Tigray kutekelezwa, wafanyikazi wa afya walizuiwa kwenda katika mkoa huo na vikosi vya usalama.

Mashuhuda wa tukio walisema kuwa watu wengi walifariki katika shambulizi la angani, na majeruhi walipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Serikali bado haijatoa maelezo zaidi juu ya shambulizi hilo la angani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...