Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, alifanya mkutano wake wa kwanza baada ya kutoka Ikulu ya White House na kuzungumzia suala la kuhesabiwa kwa kura katika uchaguzi uliopita huku akikosoa sera za Rais Joe Biden na Chama cha Democrats.
Akiwahutubia maelfu ya watu huko Wellington, Ohio, Trump alisisitiza madai yake kwamba kushindwa kwake katika uchaguzi wa Novemba 2020 kulisababishwa na ulaghai kwenye kuhesabu kura na kusema,
"Tulishinda uchaguzi mara mbili na tunaweza kuhitaji kushinda mara ya tatu. Inawezekana."
Katika hotuba yake, Rais wa zamani aligusia ongezeko la idadi ya wahamiaji wanaoingia Marekani kwa kuvuka mpaka wa kusini mwa nchi hiyo na kusema,
"Kuna mamilioni ya watu wanaokuja katika nchi yetu. Hatujui ni akina nani. Joe Biden anafanya kinyume na kile tunachofanya."
Wakati Trump alimshutumu Rais Joe Biden kwa kujipendekeza kwa China, pia alisema utendaji wake wa kazi ulikuwa wa aibu katika ulimwengu.
Kwenye mkutano huo, ambapo Donald Trump hakutoa taarifa wazi kuhusu iwapo atagombea tena au la, alitoa maneno ya kutia moyo kwa wapiga kura kwamba Chama cha Republicans kinaweza kupata tena idadi kubwa ya wanachama kwenye Baraza la Seneti la Marekani na Baraza la Wawakilishi.
Trump aliongezea kusema,
"Tutachukuwa tena bunge, seneti na utawala wa Marekani. Tutafanya hivyo hivi karibuni."

No comments:
Post a Comment