Search This Blog

Sunday, June 20, 2021

Bidhaa zisizokuwa na kiwango zakamatwa

 


Na Thabit Madai,Zanzibar.

Zaidi ya bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 200 zimekamatwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) kwa kukosa kiwango cha uingizwaji nchini pamoja na kupitiwa na muda.

Akitoa taarifa kwa wandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa  bidhaa hizo Mkaguzi Mkuu kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Suleiman Akida Ramadhani amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika maeneo ya Shakani na Kwamchina.


Alisema bidhaa hizo zimeingizwa kutokea nchini Ukrain zimeingia Zanzibar bila ya kufanyiwa ukaguzi na Wakala husika jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.

Alifahamisha kwamba bidhaa hizo hazikuwa na  vifungashio vyenye lugha inayofahamika na kutoa maelekezo pia zimeshapitwa na muda na ni hatari kwa matumizi ya binadamu.

Akizitaja bidhaa hizo nipamoja na Tambi aina ya Pasta, makoronya, sabuni mbalimbali na biskuti ambazo zimeingia nchini mwaka 2019 na hazikuwahi kukaguliwa kupitia Wakala wa  Chakula, Dawa na Vipodozi.

Mkuu huyo aliwataka wafanyabishara kufuata sheria na taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini ili kuepuka hasara pamoja na kulinda afya ya  mtumiaji.  

“Mfanya biashara yoyote ni lazima akubali maagizo anayopewa na taasisi husika kabla ya kuingiza bidhaa nchini na sio kumuachia wakala kutoa mizigo kinyemela kwani hupelekea hasara pale zitakapoangamizwa” alisema Mkaguzi huyo.

Nae Mfanyabiashra wa bidhaa hizo Ramadhani Khatibu Juma amesema amekubali kupokea uamuzi utakaotolewa na taasisi  hiyo ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kumpata mtumiaji.

Aidha alisema kuwa suala la kutokaguliwa bidhaa hizo linatokana na  kumuachia wakala wake ambaye alimthibitishia kuwa amelipia sehemu zote zinazo stahiki kulipiwa na kufanyiwa vipimo kwa matumizi ya binaadamu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...