Wanajeshi wa kikosi cha wanamajini wa Misri na Marekani (USA) walifanya zoezi la kijeshi la pamoja kusini mwa Bahari ya Shamu.
Msemaji rasmi wa Jeshi la Misri Kanali Tamir al-Rifai alisema kuwa meli za kivita za "Taba" na "Julai 18" kutoka Jeshi la Wanamaji wa Misri na "Uss Mahan", "Uscgc Charles Moulthrope" na "Uscgc Robert Goldman" kutoka Jeshi la wanamaji wa Marekani zilishiriki zoezi hilo.
Rifai alisema kuwa shughuli zilizoendeshwa kwenye zoezi hilo zilikuwa ni kama vile kuhakikisha usalama wa trafiki baharini na ulinzi wa meli muhimu za mizigo.
Akibainisha kuwa zoezi hilo lilifanywa katika upeo wa kuunga mkono usalama wa baharini katika kanda hiyo, Rifai hakujumuisha maelezo kuhusu tarehe ya kuanza au kumalizika kwa zoezi hilo katika taarifa yake.
Katika miaka ya hivi karibuni, Misri imefanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja na nchi nyingi, haswa Urusi, Ufaransa na Marekani.
Misri na Marekani pia zilifanya zoezi la kijeshi la pamoja katika Bahari ya Shammu mnamo Machi 17, 2021.

No comments:
Post a Comment