Na Maridhia Ngemela
Waziri wa Mambo ya Ndani George SimbaChawene amekemea vikali suala la askari wa Uhamiaji mkoani Mwanza,kufanya oparesheni ya kujiamulia kwa manufaa yao bila ridhaa ya ofisi ni kinyume cha taratibu na sheria za kazi.
Chawene amesema hayo mkoani Mwanza wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi,yenye lengo la kuimalisha utendaji kazi wa majeshi pamoja na ushirikiano wa wananchi katika ulinzi shirikishi.
Chawene amesema baadhi ya maafisa hufanya misako kwa masilahi yao binafsi ni dalili ya kupoteza uaminifu kwani ni vizuri ifanyike kwa uwazi kwa usimamizi na kuwa na kibali kwa sababu ya askari ambao siyo waaminifu.
"Mnafanya kazi vizuri sana na ninawapongeza,lakini kuna baadhi yenu wanafanya opatesheni za kimya kimya bila kupewa amri na ofisi na wanatenda mambo ya kudhalilisha sana hapa mkoani Mwanza,sasa watambue tumeishawabaini na muda si mrefu wataumbuka, alisema Simbachaweene.
Simba chawene amesema bado kuna kasi nzuri ya kusikiliza mashauri nitaenda kuzungumza na waziri wa katiba na sheria kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwani wafungwa wanapiga kelele humo ndani na idadi ya mahabusu inazidi idadi ya wafungwa.
Ameongeza kuwa alisikiliza wafungwa changamoto walizonazo atawasiliana na vyombo husika ili wafungwa wapate haki yao.
Kwa upande wake Mkuu wa magereza butimba Peter Anatory amesema kuwa gereza hilo linakaa na wahalifu asilimia 75.18 walioko mkoani hapa wamepewa maalekezo juu ya ulinzi na usalama na pia amewasisitiza watumishi kufuata sheria na kanuni za kazi kuzifuata ili kutenda haki.
Anatory alimshukru waziri kwa kulitembelea gereza hilo na kuweza kuzungumza na waalifu na ameweza kubaini changamoto na kuwasihii wafungwa kuishi kwa amani na upendo na kuendelea kuwa watulivu ili waweze kusubilia hukumu zao.

No comments:
Post a Comment