Nyota wa Pop Ariana Grande ameolewa na mchumba wake Dalton Gomez kwa harusi "ndogo ya faragha".
Mwimbaji huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 27 alifunga ndoa mbele ya watu wasiopungua 20 mwishoni mwa juma, shirika la habari la PA liliripoti.
Bi Grande alitangaza mnamo Desemba alikuwa alifunga uchumba na wakala wa mali isiyohamishika wa Los Angeles mwenye umri wa miaka 25.
Harusi yao ilifanyika nyumbani kwake California, kulingana na ripoti.
Mwakilishi wa mwimbaji huyo aliliambia shirika la habari la PA kuwa "Walioana. Ilikuwa harusi ndogo ya faragha ya chini ya watu 20''.

No comments:
Post a Comment