Search This Blog

Saturday, May 29, 2021

Utoaji tuzo za Oscars wasogezwa mbele


Sherehe za utoaji wa Tuzo za Oscars za msimu wa 94 zilizokuwa zimepangwa kufanyika February 27, 2022 zimesogezwa tena mbele mwezi mmoja na sasa zitafanyika March 27, 2022 sababu ikielezwa kuwa ni janga la Virusi vya Corona.

Hii sasa itakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Tuzo hizo za Oscars kuahirishwa, na ratiba mpya imetoka ya matukio yote yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Dolby Theatre huko Hollywood & Highland Center ambapo kwasasa ukumbi huo  umefungwa kutokana na janga hilo.

The Academy Awards (Oscars) Hufanyika kila mwaka na kampuni ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences (AMPAS) kwa lengo la kutambua mchango wa taaluma ya tasnia ya filamu, wakiwemo waongozaji, waigizaji, na watunzi wa filamu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...