Search This Blog

Saturday, May 29, 2021

Meya aagiza Milioni 3.2 za kununua bastola ya Mkurugenzi zirudishwe


Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza Milioni 3.2 zilizotengwa na Halmashauri ya Manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya Mkurugenzi zirejeshwe.

Raibu ametoa tamko hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Stephen Kagaigai ambaye pia alishiriki kikao hicho.

Amesema fedha hizo zilipitishwa na halmashauri hiyo mwaka 2015 na kubainisha kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Kuna fedha zilipitishwa mwaka 2015 kiasi cha Sh3.2 Milioni kwenye akaunti ya Halmashauri kununua bastola ya Mkurugenzi, haya  ni matumizi mabaya ya fedha za umma, nimeagiza fedha hizi zirudishwe mara moja,” Raibu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...