Search This Blog

Saturday, May 8, 2021

Tetesi za Soka Kimataifa leo

Chelsea na Manchester City wanataka kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 32, kutoka Bayern Munich. (ESPN)


Klabu hiyo inayoongozwa na Thomas Tuchel pia imemuongeza mshsmbulizi wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 28, katika orodha yao inapojiandaa kuimarisha safu yake ya mashambulizi msimu huu wa joto. (Bild journalist Christian Falk on Twitter)

Mshambulizi wa Brazil Neymar, 29,atasaini mkataba wa kurefusha muda wake Paris St-Germain Jumamosi ya leo, hatua itakayomfanya kusalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2026. (L'Equipe - in French)

Real Madrid wamechoshwa na Eden Hazard na wako tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa Ubelgiji aliye na umri wa miaka 30 msimu huu wa joto. (Marca)

Mkufunzi ajaye wa Roma boss Jose Mourinho ana mpango wa kubisha hodi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United kwa lengo la kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24. (Calciomercato - in Italian)

Tottenham Hotspur haina mpango wa kupokea ofa zozote za kumuuza mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, msimu huu wa joto. (Standard)

Aston Villa wanajiandaa kuwasilisha dau la £15m kumnunua winga wa Burnley wa chini ya miaka 21- Muingereza Dwight McNeil. (Football Insider)

Leicester City wana imani ya kuzipiku Liverpool na West Ham United katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard 23. (Teamtalk)

Mawakala wa Georginio Wijnaldum wanasema kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 30, angependelea kuzungumza na Bayern Munich kuhusu uhamisho wa bure baada ya kandarasi yake kumalizika Liverpool msimu huu. (Sport1 - in German)

Arsenal wanatathmini uwezekano wa kumnunua kipa Ajax na Cameroon Andre Onana,25,lakini watasubiri uamuzi wa rufaa ya marufuku ya dawa za kututumua misuli michezoni dhidi yake kabla ya kuwasilisha rasmi ofa yao (Goal)

T


ottenham na West Ham ni miongoni mwa klabu za Ulaya zinazomfuatilia mshambuliaji wa Besiktas na Canada Cyle Larin, 26. (90Min)

Everton wanataka kumsajili mlinzi wa Wigan Athletic James Carragher,18, ambaye pia ni mwana wa kiume wa mchezaji mkongwe wa Liverpool Jamie. (Telegraph)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...