Na. John Walter-Simanjiro.
Takukuru wilayani Simanjiro mkoani Manyara imemfikisha mahakamani mtendaji wa kijiji cha Rosinyai, Francis Matle kwa makosa ya kudai na kupokea rushwa ya shilingi laki moja na nusu kutoka kwa mwanachi ili aweze kumwandikia hati ya umiliki wa ardhi.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu imeeleza kuwa Kesi hiyo namba CC. 46/2021 ilifunguliwa na mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi wilayani hapo Magira Marwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo mheshimiwa Onesmo Isaac Nicodemo.
Hata hivyo Mtuhumiwa alikana mashtaka yake na alifanikiwa kupata dhamana baada ya kukidhi masharti yaliyowekwa na mahakama, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 18/5/2021.

No comments:
Post a Comment