Search This Blog

Wednesday, May 5, 2021

Serikali yatoa bilioni 5 kukabiliana na uhaba wa maji Jiji la Dodoma


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

Katika kuhakikisha inakabiliana na upungufu wa maji katika jiji la Dodoma na maeneo jirani Serikali imetoa shilingi bilioni tano (5) kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo ambapo imechimba visima vya ziada ili kuongeza upatikanaji wa maji.


Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ya kukagua hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dodoma na Wilaya ya Chamwino.

Ambapo amesema mara baada ya Serikali kuhamishia shughuli zao Dodoma na kuwa na ongezeko la watu kutokana na fulsa za makao makuu serikali imefanya jitihada za kuchimba visima ili kuongeza hali ya upatikanaji wa maji.

 “Visima 10 tayari vimeshachimbwa ikiwamo vitatu vikubwa na Wizara ya maji imeanza kutathmini mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi mkoani Dodoma na pia mradi wa bwawa la Farkwa nao upo kwenye hatua ya kuanza utekelezaji wake, lengo ni kuhakikisha Dodoma inakuwa na maji ya kutosheleza,” amesema Aweso.


Katika hatua nyingine Waziri Aweso amesema mbali na uchimbaji wa visima na kuleta maji kutoka bwawa la Farukwa Serikali inampango wa kuleta maji ya ziwa Victoria ambapo wanaanini mradi huo ukikamilika utakuwa umemaliza kabisa tatizo la maji.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Christine Ishengoma, amebainisha kuwa kamati imeridhishwa  na jitihada zilizochukuliwa na Wizara pamoja na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuhakikisha wanamaliza kero ya uhaba wa maji.

“Hatua mnazozichukua ni nzuri na zinatia moyo tunaamini kuwa tutapata maji ya kutosha katika Jiji la Dodoma na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla,” amesema.

Awali, Mkurugenzi wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, amebainisha kuwa miongoni mwa miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la Buigiri Wilaya ya Chamwino lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo milioni 2.5 ambazo zitahudumia Wilaya yote, eneo la Ikulu na mji wa kiserikli.

“Mradi huu ulikuwa na thamani ya Sh.Bilioni 2.5 lakini umetekelezwa kwa Sh.Milioni 998 kwa maelekezo ya Wizara kwamba tuhakikishe tunapunguza gharama za utekelezaji wa miradi na tumefanikiwa kwa kuwa tupo asilimia 98 ya utekelezaji wa mradi huu wa tenki,” amesema.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...