Kiongozi wa Myanmar aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi atafika mahakamani mwenyewe leo akikabiliwa na shtaka la uchochezi wa fitina.
Shtaka hilo la fitna ndilo kubwa zaidi analokabiliwa nalöo, lakini pia anatuhumiwa kwa kukkiuka sheria ya siri za serikali na kuvunja kanuni za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Suu Kyi amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mapinduzi mwanzoni mwa Februari na hajaonekana hadharani tangu wakati huo. Mawakili wake wanatumai hatimaye kumuona kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75.
Wakati Suu Kyi amekuwa akijibu maswali mahakamani kwa njia ya video katika wiki za karibuni, mawakili wake hawajaweza kukutana naye ana kwa ana.
Atafikishwa leo katika mahakama maalum iliyoundwa katika mji mkuu Naypyidaw kwa ajili ya kikao cha kusikilizwa kesi yake

No comments:
Post a Comment