Search This Blog

Sunday, May 30, 2021

Shambulizi katika harusi nchini Afghanistan


Raia 7 wameuawa katika shambulizi la Taliban katika mkoa wa Kapisa nchini Afghanistan.


Msemaji wa Idara ya Polisi ya Kapisa Shayık Shurish amesema kuwa wanamgambo wa Taliban walishambulia harusi katika kijiji cha Enarcuy.


Akiripoti kuwa raia 7 wamepoteza maisha na raia 4 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo, Shurish amesema kuwa watoto walikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha.


Taliban kwa upande wao wamedai kuwa shambulizi hilo la lilitekelezwa na vikosi vya usalama.


Kwa upande mmoja, juhudi za kuhakikisha utulivu nchini zikiwa zinaendelea,  mashambulizi nayo yamepamba moto.


Mbali na hapo, kulingana na serikali ya Afghanistan ghasia zimeongezeka nchini tangu majeshi ya kigeni yalipoanza kujiondoa kwa takriban mwezi mmoja.


Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) wametangaza kuwa raia 573 waliuawa nchini Afghanistan katika robo ya kwanza ya mwaka 2021.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...