Search This Blog

Saturday, May 8, 2021

Serikali yasitisha ukaguzi wa nyimbo za wasanii

Serikali ya Tanzania imesitisha utekelezaji wa kanuni za kukagua nyimbo za wasanii kabla hazijapelekwa kwenye redio, televisheni na majukwaa mbalimbali.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumamosi Mei 8, 2021 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa alipokutana na wadau wa muziki nchini wakiwemo wasanii mkoani Dar es Salaam.

Kanuni hizo ni za sheria namba 23 ya mwaka 1984 ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2019. Kanuni hizo namba 25 kifungu (1)-(8) inaeleza kuhusu masharti mahususi  juu ya masuala ya maadili ya kazi za sanaa na utoaji wa ithibati katika kazi za sanaa.

Bashungwa amechukua uamuzi huo baada ya wadau wa muziki kupinga suala hilo wakidai haliwatendei haki ikiwa ni baada ya Basata kuzuia wimbo wa Mama wa msanii Ney wa Mitego kwa maelezo kuwa una mashairi yenye ukakasi.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...