Search This Blog

Saturday, May 8, 2021

IGP Sirro azungumzia agizo la Mhe. Rais alilolitoa wakati akizungumza na Wazee

 


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kutoa taarifa kwa Jeshi hilo huku akiwaagiza Wenyeviti wa serikali za Mitaa kusaidiana na Polisi Kata kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyosaidia kukomesha vitendo ya kihalifu katika maeneo yao.

IGP Sirro amesema hayo wakati akiongea na Maofisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam huku akiwapa mwezi mmoja kuhakikisha wanakomesha vitendo vya uhalifu katika jiji hilo. 

IGP Sirro aliitoa kauli hiyo Kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati akizungumza na Wazee wa jiji la Dar es salaam na alipotoa agizo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kukomesha vitendo vya ujambazi katika jiji hilo.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kusisitiza hasa kwa watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani ambapo amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutumia sheria zilizopo ili kuwadhibiti.

Pia alisema kuwa Jeshi hilo litaendelea kuangalia mamlaka zilizopo kuhusu wale wanaotoka gerezani kwa rufaa na Jeshi la Polisi limetaka kushirikishwa ili kuhakikisha kwamba mtu anayetolewa awe amebadilika tabia na kutokuwa kero/tatizo kwa Watanzania pindi anapopata msamaha huo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...