Saudi Arabia itaandaa ibada ya Hijja ya Makka kwa mwaka huu lakini kwa mazingira maalumu, yenye kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Covid-19.
Habari hiyo ni kwa mujibu wa televisheni ya umma.Ikieleza kwa kunukuu wizara ya inayohusika na hijja televisheni hiyo ilieleza kwamba utaratibu na masharti ya kufanikisha ibada hiyo utatangazwa katika kipindi kijacho.
Mwaka uliopita, Saudi Arabia iliruhusu idadi ndogo ya mahujaji wa ndani ya taifa hilo kutokana na kuzuka kwa janga la virusi vya corona.

No comments:
Post a Comment