Mataifa ya Kiarabu, yakiwemo manne ambayo mwaka uliopita yakubali kurekebisha uhusiano wao na Israeli, yamezilaani ghasia za mwishoni mwa juma ambazo zilisababisha mamia ya Wapalestina wajeruhiwe baada ya makabiliano na vikosi vya usalama vya Israel.
Ukosoaji wa kutokana na vitendo vya Israel umetolewa na mataifa ya Sudan, Morocco, Jumuiya ya Falme za Kiarabu na Bahrain, yote kwa pamoja mwaka uliopita yalikubali kurejesha mahusiano ya kidiplomasia na Israel.
Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nchi za nje ya Sudan imeiviita vitendo vya Israel dhidi ya Wapalestina mjini Jerusalem kuwa ni vya ukandamizaji na kimabavu.
Vurugu hizi za sasa katika maeneo ya msikiti wa Al-Aqsa huko mashariki mwa Jerusalem, zinatajwa kuwa mbaya zaidi kutokea tangu 2017, zinachochewa na jitihada ya muda mrefu ya walowezi wa Kiyahudi za kuchukua nyumba za Wapalestina.

No comments:
Post a Comment