Search This Blog

Wednesday, May 26, 2021

Rwanda: Mtetemeko wa ardhi wawalazimu mamia kutoroka makwao


Mamia ya watu wanasadikiwa kutoroka makwao siku ya Jumanne katika mji wa Gisenyi Magharibi mwa Rwanda kufuatia mitetemeko ya ardhi inayoshuhudiwa kwa siku ya nne baada ya mlipuko wa volkano nchi jirani ya DR Congo.

Kifaa cha kufuatilia matetemeko ya ardhi nchini Rwanda kimeripoti matetemeko ya ardhi yaliyofikia kiwango cha 5.3 na 5.1 katika vipimo vya richa Jumanne na Jumatano asubuhi.

Mamlaka nchini Rwanda imetoa wito wa utulivu na kusema kuwa imechukua hatua ya kuwasaidia watu waliyo katika hali ya hatari, baada ya nyumba kadhaa kuharibiwa.

Shule, benki, soko na maduka yamefungwa, huku watu wakilala nje usiku wa Jumanne kwa kuhofia nyumba zao kuporomoka na kuwaangukia.

Baadhi ya watu walionekana Jumatano asubuhi katika kituo kikuu cha usafiri wakijaribu kuondoka Gisenyi kuelekea maeneo ya mashariki.

Watu walionekana katika vituo vya usafiri wakijaribu kuondoka mji huoImage caption: Watu walionekana katika vituo vya usafiri wakijaribu kuondoka mji huo

Hospitali katika mji huo zilihamisha baadhi ya huduma na wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika maeneo yam engine ya magharibi na kaskazini mwa Rwanda.

Bi Mwajuma Gakuru ameomba srikali imsaidie baada ya nyumba zake kuharibiwa katika mtetemeko wa ardhi wa Jumanne

“Hali ni mbaya sana, tuna hofu tangu (mlipuko wa volcano) Jumamosi,anhalia nyumba zangu, zote,tunaomba serikali itusaidie .” – alisema.






No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...