Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewataka wakurugenzi wa halmashauri zilizopo mkoani humo wampelekee taarifa za matumizi ya fedha za mfuko wa elimu.
Zambi ametoa agizo hilo leo wakati wa mkutano maalum wa wadau wa mazao ya korosho na ufuta. Kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa iliyopo katika manispaa ya Lindi.
Zambi alisema kuna matumizi ya fedha yasiyoridhisha za mfuko huo. Hasa katika eneo la mgao wa fedha katika utekelezaji wa miradi mbali mbali.
Alisema kumekuwa na mgao unaosababisha baadhi ya miradi kukwama. Hali ambayo inasababisha kutokuwepo matokeo mazuri ya utekelezaji miradi hiyo.
'' Kuna halmashauri zinapata fedha nyingi lakini hazina mgawanyo mzuri katika kutekeleza miradi,'' Zambi alibainisha.
Katika kuhakikisha kwamba agizo hilo linafanyiwa kazi haraka, alisema utekelezaji ufanyike ndani ya mwezi huu wa Mei. Nakwamba ziwe zimefikishwa kwa katibu tawala wa mkoa(RAS) wa Lindi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi ametoa wito kwa wenyeviti wa halmashauri wawe mstari mbele kuhamasisha uchangiaji masuala ya elimu.
Huku akionya kwamba nijambo lisilokubalika kwa viongozi kuwa sehemu ya vikwazo katika kuchangia sekta ya elimu.
Mbali na hayo, wajumbe wa mkutano huo walikubaliana kwa kauli moja kwamba ununuzi wa ufuta uanze tarehe 29.05.2021. Nakwamba tarehe hiyo maghala yaanze kupokea ufuta kwa ajili ya ununuzi.

No comments:
Post a Comment