Search This Blog

Wednesday, May 19, 2021

Rais Samia afanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa miwili aliowateua


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Mei 19, 2021, amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa miwili aliowateua hivi karibuni.

David Kafulila anakwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu badala ya Arusha kama alivyoteuliwa awali, akichukua nafasi ya John Mongella.

Aidha Rais Samia amembadilisha John Mongella kutoka kuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Kabla ya kuteuliwa kwenda Simiyu Mongella alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Rais Samia amesema sababu ya mabadiliko hayo ni uzoefu wa Mongella kuongoza jiji la Mwanza hivyo inabidi akaongoze jiji la Arusha ili Kafulila ambaye ndio anashika nafasi hiyo kwa mara ya kwanza aanzie Simiyu.

Mabadiliko hayo ameyafanya wakati akitoa hotuba baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa wateule na wakuu wa taasisi mbalimbali, Ikulu Dar es salaam.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...