Search This Blog

Wednesday, May 19, 2021

Namibia yaruhusu kuingia kwa mabinti pacha wapenzi wa jinsia


Namibia yaruhusu kuingia kwa mabinti pacha wa wapenzi wa jinsia moja nchini humo Namibia imetoa stakabadhi za usafiri kwa watoto pacha wa kike wa wanandoa wa jinsia moja ambao wamekuwa wakipigana mahakamani kuwapeleka nyumbani kutoka Afrika Kusini walikozaliwa.

Wizara ya maswala ya ndani ya Namibia, ambayo ilithibitisha kutoa hati hizo, hata hivyo ilisema hatua hiyo haikuwapa uraia pacha hao. Phillip Lühl, raia wa Namibia, na mumewe wa Mexico Guillermo Delgado wamekuwa wakipigania uraia wa Namibia kwa binti zao, ambao walizaliwa mnamo Machi kwa mwanamke wa kujitolea nchini Afrika Kusini.

Pacha hao walikataliwa kuingia Namibia mnamo Aprili - na maafisa walimtaka Bwana Lühl athibitishe kupitia DNA kuwa ndiye baba wa watoto hao.

Walakini waziri mpya aliyeteuliwa mnamo Aprili, Albert Kawama, alisoma hati za hapo awali na "kuidhinisha kutolewa kwa vyeti vya dharura vilivyoombwa", shirika la habari la AFP linaripoti.

Wanandoa hao wamepokea uamuzi huo, lakini waligundua kuwa ulivuruga familia yao . Namibia imepiga marufuku mahusiano ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja lakini sheria hiyo huwa haitekelezwi



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...