Search This Blog

Thursday, May 6, 2021

MV Mwanza kukamilika mwakani

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho   amesema ujenzi wa  Meli ya Mv Mwanza Hapakazi tu ambao hadi sasa umefikia asilimia 74 utakamilika baadaye mwakani.

 


Waziri Chamuriho ameyasema hayo leo jijini Mwanza alipokuwa akikagua ujenzi wa meli hiyo ya kisasa  inayojengwa na Kampuni ya Gas Ente kutoka Korea ya kusini ikishirikiana na Kaang Nam Corperation pamoja na Suma JKT.

 Aidha Waziri Chamuriho amesema ujenzi wa meli hiyo ni moja  ya miradi mikubwa minne inayotekelezwa na   kampuni ya huduma za Meli  Nchini (MSCL) na kusimamiwa na  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. 

 


“Miradi  mengine inayotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa  ni pamoja na ukarabati  wa Meli ya New Victoria,Ujenzi wa MV Butiama pamoja na Chelezo  ambayo ujenzi wake umekamilika”, amesema Chamuriho.

 Katika hatua nyingine Waziri Chamuriho amesema Wizara pia imejipanga kuendeleza miradi mingine katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa ikiwemo mradi wa Ukarabati wa meli kongwe ya MV Liyemba .

 Kwa upande wake Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Mv Mwanza  Mhandisi Vitus Mapunda amesema  Ujenzi huo umeajiri Zaidi ya watumishi 180 katika kada mbalimbali  na utakapokamilika utaleta fursa nyingi za ajira nchini.

 


Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL) Philemon  Bagambilana amesema  kampuni imejipanga kuboresha  na kutoa huduma  bora katika  usafiri  wa majini kwenye Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na kupanua huduma kwenye  Bahari ya Hindi.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...