Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa, ameishauri serikali kujenga nyumba Jijini Dodoma ambazo watawekeana mkataba wa miaka mitano na mbunge atakayekuwepo na iwapo ikitokea mbunge haendelei tena kuwa mbunge hiyo basi nyumba hiyo atakaa mbunge mpya atakayekuja.
Kawawa ametoa ushauri huo hii leo Mei 31, 2021, Bungeni Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo swali lake alililelekeza Wizara ya Ujenzi juu ya umuhimu wa kujenga nyumba kwa ajili ya wabunge, ambapo Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara, aliahidi kuufanyia kazi ushauri huo.
"Kwanini serikali isijenge nyumba ambazo watakuwa wanaweka mkataba kwa wabunge kila baada ya miaka mitano ambao wanaendelea, wataendelea kukaa kwenye nyumba hizo lakini ambao watakuwa hawaendelei basi wabunge wapya watakaa kwenye hizo nyumba," ameuliza Mbunge Kawawa.

No comments:
Post a Comment