Search This Blog

Sunday, May 23, 2021

Mashindano yamalizika kwa maafa China

 


Mashindano ya mbio yamemalizika kwa maafa nchini China.


Washindani 21 wamepoteza maisha yao kutokana na hali mbaya ya  hewa katika mbio za kilometa 100, ambazo pia zilijumuisha kupanda mlima.


Katika marathoni iliyoanza katika jimbo la Gansu Jumamosi asubuhi, wanariadha 172 walianza kukimbia kama ishara ya kuanza.


Walakini, wakati wa mbio za kilometa 100, hali ya hewa ilizorota ghafla, ikawa baridi na mvua ikaanza kunyesha, na kupelekea wanariadha kukwama katika eneo hilo


Baada ya hali hiyo kutokea , operesheni ya kuokoa wanariadha ilianza.


Wanariadha 151 kati ya 172 wameokolewa, wakati 21 wamepoteza maisha.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...