Rais wa Marekani (USA) Joe Biden, alisisitiza kuwa hakutakuwa na mabadiliko katika ahadi zao za usalama kwa Israel.
Biden alitoa taarifa iliyosema,
"Hakutakuwa na amani mpaka nchi za kanda zitambue haki ya Israel ya kuishi kama nchi huru ya Kiyahudi."
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya kikako cha pande mbili pamoja na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, Biden alizugumzia mashambulizi ya Israel huko Gaza na suala la dola milioni 735 katika uuzaji wa silaha kwa Israel kwa kujibu ukosolewaji na baadhi ya duru za Kidemokrasia.
Biden aliogezea kusema,
"Hakuna mabadiliko katika ahadi zangu kwa usalama wa Israel. Bado tunahitaji suluhisho la serikali mbili katika eneo hili, na hii itakuwa suluhisho pekee la mzozo."
Akibainisha kuwa watafanya kazi katika kuunda kifurushi cha uchumi na nchi zingine kwa ujenzi wa Gaza, Biden pia alisema,
"Hakutakuwa na amani mpaka nchi za kanda zitambue haki ya Israel ya kuishi kama nchi huru ya Kiyahudi."
No comments:
Post a Comment