Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.Image caption: Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.
Marekani imeweka vikwazo kadhaa vya kiuchumi na usaidizi wa kiusalama dhidi ya Ethiopia kufuatia mzozo wa eneo la Tigray.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, pia ametangaza marufuku usafiri dhidi ya maafisa wa Ethiopia na Eritrean o pamoja na wengine ambap wanatuhumiwa kufanya ukatili.
Bw. Blinken amesisitiza kuwa hatua ya kimataifa inahitajika ili kusaidia katika utatuzi wa mzozo huo na kuongeza kuwa wale waliopewa dhamana hawajachukua hatua madhubutikukomesha uhasama.
Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.
Pande zote mbili zimelaumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mapema siku ya Jumapili serikali ya Ethiopia ilipuuzilia mbali madai kwamba raia katika eneo lililokumbwa na vita la Tigray walilengwa kwa silaha za kemikali kutoka kwa majeshi ya Ethiopia au Eritrea.
Gazeti la Telegraph la Uingereza limeripoti kuwa watu kadhaa walichomeka vibaya kutokana na utumizi ya phosphorous nyeupe. Kemikali ambayo inaweza kutumika kihalalli vitani lakini ikitumiwa dhidi ya raia inasadikiwa kuwa uhalifu wa kivita.

No comments:
Post a Comment