Search This Blog

Sunday, May 23, 2021

Maelfu waandamana Ufaransa kuwaunga mkono Wapalestina

 


Maelfu ya watu waliandamana jana Jumamosi mjini Paris na katika miji mingine ya Ufaransa kuwaunga mkono Wapalestina kufuatia mgogoro wa Mashariki ya kati baina ya Israel na Wapalestina.

Chama cha wafanyakazi CGT kimesema takriban watu 4,000 walishiriki maandamano hayo mjini Paris.

Maandamano pia yalifanyika katika miji ya Lyon, Strasbourg, Toulouse na Montpellier kusini mwa nchi hiyo.

Nchini Ujerumani, mamia ya waandamanaji pia walijitokeza katika miji kadhaa jana kuwaunga mkono Wapalestina.Polisi imesema usiku wa kuamkia leo kwamba maandamano hayo iliyoshuhudiwa katika miji ya Berlin, Frankfurt, Giessen na Leipzig, yalifanyika kwa amani.

Awali Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alionya dhidi ya matamshi ya chuki au matendo ya ubaguzi wa rangi kwenye maandamano hayo kwamba kuchochea chuki dhidi ya Wayahudi na kwa misingi ya ubaguzi wa rangi ni kinyume cha sheria, na matendo kama hayo ni lazima yaadhibiwe vikali.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...